.

1/14/2019

Ukweli kuhusu Christian Bella kufunga ndoa


Hivi karibauni kulisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Christian Bella akiwa katika muonekano kama amefunga ndoa na kuibua maswali mengi.

Sasa meneja wa muimbaji huyp akizungumza na Clouds FM amesema kuwa picha zilizosambaa ilikuwa ni kwa ajili ya kutengeneza video mpya ya Bella na AY na Mwana FA.

"Hii ni video ya ngoma yake mpya inaitwa Namvisha Pete ambayo amewashirika wasanii AY na MwanaFA,  kwa ajili ya kuboresha tukaamua kufanya video ya harusi, haikuwa kiki ni kazi,’’ amesema King Dodoo.

Ukiachana na AY na Mwana FA, Christian Bella amefanya kazi na wasanii kadhaa wa hip hop Bongo kama Fid na Weusi.