F VIDEO: Wanafunzi wa Sekondari wakatisha masomo, Kisa .. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

VIDEO: Wanafunzi wa Sekondari wakatisha masomo, Kisa ..


Kufuatia changamoto ya Umbali wa kusafiri kilomita 7 kwenda na Kurudi ili kupata wa Elimu ya sekondari katika Kijiji cha Kinko kata ya Lukozi Wilayani Lushoto Mkoani Tanga Wengi wa wanafunzi wanalazimika kukatiza masomo yao kutokana na tatizo hilo.

Akizungumza Mwenyekiti msaafu wa Kijiji cha Kinko kata ya Lukozi Bwana Charles Mavoa amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto hizo pia elimu kwa mtoto wa kike imekuwa tatizo hivyo wengi kulazimika kukatiza masomo yao na kutoroka kusikojulikana na kwenda kufanya kazi mjini.

Amesema kuwa Shule ya Msingi ipo na watoto wanakwenda shule lakini upatikanaji wa elimu ya sekondari bado ni tatizo sugu kutokana na wengi kusafiri umbali wa kilomita zaidi ya 6 kwenda kufuata elimu hiyo ya kidato cha kwanza.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUSCRIBE