Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Wakandarasi wanaojenga miundombinu ya maji katika vijiji vya Chimbendenga,Mtua na Ndomoni katika halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,mkoa wa Lindi wameombwa kuendelea na kazi wakati madai yao ya malipo yanashugulikiwa.
Wito huo kwa wakandasi hao umetolewa na Mkuu wa Idara ya maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Sultani Ndoliwa kwenye kikao cha baraza la madiwai,kilichofanyika leo mjini Nachingwea.
Mhandisi Ndoliwa alisema wakandarasi hao hawanabudi kuendelea nakazi katika kipindi hiki ambacho serikali inashugulikia malipo waliyoomba kutokana na kazi walizofanya katika miradi hiyo.
Alisema nikweli wakandarasi wanaojenga miundombinu katika vijiji hivyo hawajalipwa tangu waanze kujenga.Huku baadhi yao wakiwa wamejenga kwa asilimia 80 ya kazi walizopewa.Hata hivyo waendelee na kazi kwani malipo yao watapata kipindi kifupi kijacho.
"Wakandarasi wanaojenga katika vijiji vya Chimbendenga,Mtua na Ndomoni wamejitahidi sana.Wengine wametekeleza 80 ya kazi.Lakini mkandarasi anaejenga mradi wa Mandawa kasi yake hairidhishi,"alisema Ndoliwa.
Mkuu huyo wa idara ya maji alibainisha kwamba wakandarasi hao wanaojenga miradi mitatu kati ya minne tangu mwezi Desemba,mwaka jana kasi yao ya ujenzi imekuwa ndogo.Huku wote wakiwa wameomba malipo ya kazi walizofanya.
Alisema hali hiyo inaashiria kwamba kusuasua kwao kuendelea na kazi kunasababishwa na kutolipwa madai yao yenye thamani ya shilingi 230.00 milioni kati ya shilingi 837.00 milioni ambazo ni gharama ya miradi yote minne.
Hata hivyo Ndoliwa alisema mkandarasi anayetejenga katika kijiji cha Mandawa,kata na tarafa ya Ruponda kasi yake ujenzi hairidhishi tangu alipoanza kazi hadi sasa.Hivyo watakutananae ili wamuulize kama bado anania yakuendelea na kazi au ameshindwa.
"Kwamujibu wa mikataba nikwamba ujenzi ulitakiwa umalizike tarehe 15,mwezi huu.Hata hivyo tumeongeza miezi mitatu kutokana na changamoto hiyo ya malipo,"aliongeza kusema Ndoliwa.
Awali baadhi ya Madiwani,hasa ambao miradi hiyo inatelezwa kwenye kata zao walihoji sababu za miradi hiyo kusuasua ujenzi wake.Hali ambayo ni tofauti na awali wakati wakandarasi wanaanza kujenga.
