Waziri Mkuu ampa agizo hili Waziri Ummy Mwalimu


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kassim Majaliwa leo amefanya ziara katika mji mpya wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ihumwa jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya shughuli za ujenzi ambazo zinatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Januari 2019.

Katika ziara hiyo, Majaliwa amemwagiza Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi, na kuongeza idadi ya wafanyakazi ili kuhakikisha anamaliza kazi yake ifikapo Januari 31, 2019 na kukabidhi kwa Wizara ya Afya ili waendelee na majukumu yao ya kuboresha Sekta ya Afya.

Aidha, amemwagiza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusimamia kikamilifu ujenzi wa jengo hilo kila siku ili kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika ndani ya muda waliokubaliana, kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.

"Mhe. Waziri hawa wanatakiwa kusimamiwa kila siku, hili ndio jengo lililochini, ukiondoa lile la Waziri Mkuu ambalo wameanza kazi jana, hili ndio lipo chini na ndio la wale wale Mzinga, Kamanda lisije lilakuahibisha hili" alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.