.

2/14/2019

Abdu Kiba atamani kumfikia Alikiba


Msanii wa muziki Bongo Fleva, Abdu Kiba amesema anaaamini siku moja atafikia pale alipofika kaka yake, Alikiba kimuziki.

Muimbaji huyo akizungumza na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV amesema
hakuna kinachoshindikana na anajiona kufika mbali zaidi.

"Chini ya jua hakuna kinachoshindikana ajuaye siri ni Mungu, ila wote tuna imani tufike
walipofika wasanii wengine kama alivyofika kaka yangu Alikiba," ameeleza.

"Ni muujiza utatokea muda wowote ni nia na ubora wa kazi zako nina imani jicho langu
linaona mbali nitafika alipofika ndugu yangu,’’ amesema Abdu Kiba.

Kwa sasa muimbaji huyo kutokea lebo ya King's Music anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Mubashara.