AS Roma yamtaka Maurizio Sarri

Klabu ya AS Roma imefanya mawasiliano na wawakilishi wa Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri kuangalia kama atapenda kuwa kocha wa timu hiyo ya Itali kwa msimu ujao.

Sarri ambaye yupo kwenye wakati mgumu kwenye klabu ya Chelsea baada ya kupata matokeo mabaya kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City ambapo walipokea kipigo cha mabao 6-0 na baadaye kutupwa nje kwenye kombe la FA na  Manchester United.

Roma wanamuhitaji Sarri baada ya kuona timu hiyo ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa Serie A na kupokea kipigo cha bao 7-1 kutoka kwa Fiorentina kwenye robo fainali ya Coppa Italia.