Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nistahi na Maji (EWURA) imesema bei za mafuta yanayopitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa mwezi wa pili mfululizo na kufikia Tsh. 2,120 kwa lita moja ya petroli, 2,080 kwa dizeli na 2,046 kwa mafuta ya taa.
Taarifa ya Mamlaka hiyo imeeleza kuwa bei hizo zitaanza kutumika Leo Februari 6 na Kwa kila lita kumekuwa na punguzo la Tsh. 175 kwa petroli, Tsh. 144 kwa dizeli na Tsh. 156 kwa mafuta ya taa,
Pia kwa mwezi Januari na Februari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa jumla ya Tsh. 316, Tsh. 356 na Tsh. 323, mtawalia.
Hata hivyo taarifa hiyo imeeleza bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Tanga zitaendelea kuwa zile za mwezi uliopita kwa sababu hakukuwa na shehena mpya, halkadhalika bandari ya Mtwara zitaendelea kuwa zile zile zilizotangazwa Januari 25 2019, ambapo petroli ilipungua kwa shilingi 271 na dizeli shilingi 221 kwa lita.
