Bilionea Mo Dewji atoa kauli kufuatia matokeo mabovu ya Simba SC


Mfanyabishara maarufu nchini na Mwekezaji ndani ya Timu ya Simba SC, Mohammed Dewji amesema bado hajakata tamaa licha ya timu hiyo kupata matokea mabovu.

Utakumbuka Jumamosi iliyopita Wekundu wa msimbazi, Simba SC walijikuta wakiambulia kipigo kizito cha goli 5-1 kutoka kwa Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabigwa Barani Afrika.

''Roho yangu bado inaniuma. Naipenda sana Simba, na bado sijakata tamaa. Roma haikujengwa kwa siku moja,'' ameeleza Mo Dewji.
Hadi sasa Simba SC ina pointi tatu katika michezo mitatu iliyocheza, ikiwa imefunga magoli matatu pekee, huku ikiruhusu jumla ya magoli 10 katika michezo miwili ya mwisho kucheza dhidi ya AS Vita kutoka DR Congo na Al Ahly ya Misri.

Mfanyabisha Mo Dewji anaumiliki wa hisa wa asilimia 51 ndani ya Simba SC, huku asilimia 49 ikibaki kwa wanachama. Kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes linaeleza kuwa utajiri wa wa kijana huyu kufikia US Dollar Bilioni 1.5.