Bunge la Misri laridhia Rais kuongoza hadi 2034


Bunge la Misri limepiga kura na kuridhia mabadiliko ya katiba ambayo yatamwezesha Rais
Abdel Fattah al-Sisi kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034, pindi mchakato huo
utakapokamilika.

Mabadiliko hayo pia yataongeza muda wa Rais kuongoza kutoka miaka minne kwa muhula, hadi
miaka sita.

May 2014 ndipo Abdel-Fattah al-Sisi alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo. al-Sisi
aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini humo.

Hivi karibuni al-Sisi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa nchi huru za
Afrika (AU).Hii baada ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame kumaliza kipindi cha Ungozi wake kilichodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.