Gari la Zima Moto lawasili Bungeni baada ya taharuki


Leo Mwenyekiti wa Bunge Najma Giga amelazimika kuahirisha kwa muda kikao cha Bunge kilochokuwa kikiendelea kutokana na alarm ya tahadhari kulia kwenye jengo hilo na kusababisha taharuki.

Baada ya taharuki hiyo maafisa wa zimamoto na maofisa wengine wa usalama wameshafika eneo la ukumbi wa Bunge kujua nini hasa kimetokea, kwa sasa inaelezwa hali imetulia na wabunge wanaendelea na shughuli zao.

Mkutano wa 14 wa Bunge La 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulianza Januari 29, 2019 Jijini Dodoma ambapo unatarajiwa kuisha wiki hii. Kaa karibu na Muungwana Blog kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.