.

2/10/2019

Habari njema kwa mashabiki wa Manchester United

Mchezaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani, huenda akaukosa mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 ya Ligi ya Mbingwa Ulaya dhidi ya Manchester United.

Cavani mwenye miaka 31 huenda akaukosa mchezo huo baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi ya Ufaransa dhidi ya Bordeaux ambapo PSG ilishinda kwa bao 1-0.

Kwa hali hiyo PSG inazidi kupata pigo kwani hadi Neymar naye ataukosa mchezo huo kwa sababu ya kuwa majeruhi.