Harmonize afika Polisi, Ni suala la bangi liloibuliwa na RC Makonda


Msanii wa muziki Bongo, Harmonize leo amefika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaa kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuvuta bangi.

Muimbaji huyo kutokea kwenye lebo ya WCB amefika kituo hapo majira ya saa mbili kama alivyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Utakumbuka January 31, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikutana na wasanii wa muziki na filamu nchini ili kujua changamoto zao.

Katika mkutano huo, RC Makonda aliibua suala kuhusu msanii huyo kuwa anawasi wasi huenda akawa anavuta bangi, hivyo alitaka achunguzwe.

Hii ni baada ya muimbaji huyo kuchapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa nchini Ghana ikimuonyesha akivuta kitu kinachohisiwa kuwa ni bangi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items