Helikopta yaanguka watatu wafariki na wengine wajeruhiwa

Helikopta ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha ulinzi wa amani inayomilikiwa na Ethiopia yaanguka mji wa Abyei nchini Sudan. Watu 3 wapoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa.

Kikosi cha muda cha ulinzi wa amani cha Umoja wa mataifa eneo lenye mgogoro  kusini mwa Sudan  katika mji wa Abyei (UNISFA) kimetoa taarifa kwamba helikopta ya Ethiopia aina "Mi-8" iliyokuwa imebeba watu 23 imeanguaka makao makuu ya UNISFA. Katika tukio hilo 3 wamefariki, 3 wamejeruhiwa vibaya na wengine 10 wana majeraha madogo.

Ethiopia inashiriki ulinzi wa amani kwa kushirikiana na UNISFA katika eneo la Abyei. Na ina jumla ya wafanyakazi 4, 500 katika eneo hilo.

Sudan pamoja na Sudan ya kusini kila moja anadai kwamba eneo la Abyei ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta ni mali yake.