Kazi ya Jeshi la Polisi lafananishwa na ya Wachungaji


Na Timothy Itembe Mara,

JESHI la polisi limetakiwa kumsaidia Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufu kazi kwasababu jeshi hilo lipo kisheria na linatakiwa kufanya kazi kwa weredi kwa kuzingatia masomo wanayoyapata pindi wakiwa Chuoni.

Kauli hiyo ilitolewa jana kwenye maafali ya tatu ya wahitimu ngazi ya cheti ya wachungaji na Bishop Petro Kasululu ambaye pia ni mkurugenzi wa Chuo cha East Africa Christian College kilichopo Mjini Tarime mkoani Mara.

"Chuo chetu kinatambulika na serikali inakitambua hata haya tunayoyafanya serikali inajua vinginevyo wangetukamata kama tungekuwa tumekiuka sheria kwa hali hiyo nawaomba jeshi la polisi kufanya kazi kwa weredi na kuzingatia pia mafunzo mnayoyapata katika vyuo vyenu kwasababu kazi yenu inafanana na kazi ya wachungaji katika kuponya watu majereha yao sisi tunaponya kiroho ninyi mnaponya kimwili na katika kufanya hivyo mtakuwa mnamsaidia kazi Rais wetu John Pombe Magufuli"alisema Kasululu.

Pia Kasuslulu aliongeza kwa kusoma moja ya kitabu cha Bblia Petero wa kwanza Moja msitari wa tano  hadi wa sita ambapo alisema kuwa basi nyenyekeeni kwa mkono wa Bwana uliohodari na katika kufanya hivyo mtakuwa mnatenda yaliyokweli bila uonevu.

Kwa upande wake mgeni rasimi kwa niaba ya mkuu wa polisi mkoa Tarime Rorya,Henry Mwaibambe mkuu wa kituo cha polisi Tarime mjini,SSP Wilison Mlowola alisema kuwa waunmini wa kanisa ni watumishi wa Mungu kwa hali hiyo nendeni kwa jamii mkafanye yale yote mnaojifunza makanisani pamoja na vyuo ili kuondokana na maovu huku mkuwahudumia watu kwa kuzingatia sheria za haki za binadamu huku mkihofu kutenda dhambi pamoja na kusaidia jamii ili kitii  sheria za serikali zilizopo.

Akisoma risala kwa mgeni rasimi mmoja wa wanachuo kumi waliohitimu mafunzo ngazi ya cheti katika chuo hicho,Damari Emanuel alisema kuwa maafali hayo ni yatatu tangu chuo kuianza ambapo chuo kilianza mwaka 2016 na kuwa wamehitimu wakiwa wanafunzi  kumi wamehitimu mafunzo ngazi ya cheti kati yao akiwemo yeye mwanamke pekee huku wengine wakiwa wanaume.