Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia Congo Martin Fayulu amekataa juhudi za rais mpya wa nchi hiyo Felix Tshisekedi za kutaka maridhiano.
Wito huo wamaridhiano umetolewa na Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika jitihada ya kutafuta maridhiano ya kisiasa nchini humo. Fayulu amesema pale unapopewa mkono ambao ni mchafu, hupaswi kuupokea.
Kwenye hotuba yake rasmi ya kwanza tangu kushindwa kwenye uchaguzi wa rais, Fayulu aliwaambia mamia ya wafuasi wake waliokusanyika mjini Kinshasa, kuwa awasifanye fujo wakati anapoendelea kupinga uchaguzi anaodai ulikumbwa na udanganyifu. Kiongozi huyo wa upinzani amehimiza Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kutopokea maagizo kutoka kwa mtu anayedai kuwa Wakongo hawakumchagua.
