Kocha wa Manchester City kupambana mwanafunzi wake Leo


leo Arsenal ya kocha Unai Emery's itakuwa Uwanja wa Etihad kumenyana na Manchester City ya Pep Guadiola, kocha wa Arsenal amesema  Guadiola ni mwalimu wake kwani anajifunza vitu vingi kupitia kwake.

"Huwa najifunza mengi nikiangalia timu za Guadiola kuanzia Barcelona, Bayern Munich na City zote zilikuwa na wachezaji wazuri ila sifa kubwa ya Guadiola ni kuinoa kiwango chao. Kwa kweli yupo juu ya makocha wengine ulimwenguni.

Kocha wa Man City, Guardiola ameonya kuwa baada ya timu yake kufungwa na Newcastel watakuwa tofauti dhidi ya Arsenal.

Guardiola amesema wamechambua kwa kina makosa waliyofanya kwenye mechi yao iliyopita na Newcastle kwa kila hatua hawatarudia makosa hayo kwenye mechi yao dhidi ya Arsenal.




Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items