Taasisi ya mambo ya anga Nasa yagundua pengo kubwa la barafu katika bara la Antaktika

Magharibi mwa bara la Antaktika chini ya barafu za Thwaities inawezekana limegunduliwa pengo la barafu lenye ukubwa wa tani bilioni 14.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na NASA zinasema chini ya barafu za Thwaites pengo kubwa lenye kimo cha mita 300 limegunduliwa.

Mtafiti katika maabara ya NASA Pietro Milillo, amesema kuwapo kwa pengo kubwa kiasi hicho chini ya barafu kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuyeyuka kwa barafu.

Kuyeyuka kwa barafu za Thwaites kumechangia kupanda kwa kina cha bahari kwa asilimia 4.

Habari za kina kuhusu utafiti huo zimechapishwa katika jarida la "Science Advances"
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items