Kisa Pete: Kijana auawa kwa kukatwa shingo


Hatika hali isiyo ya kawaida, kijana Samson Conrad mwenye umri wa miaka 24 ameuawa kwa kukatwa na sime shingoni na Kereto Lekoko.

Kisa cha ugomvi huo inaelezwa kuwa wawili hao Walikuwa wakidaiana pete.Samson Conrad alifariki
baada ya kuvuja damu nyingi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

Amesema wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa alitaka kupatiwa fedha yake, na ndipo alipochomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni.