Msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB, Mbosso ameweka wazi ukaribu wake na msanii mwenzake, Aslay ambaye awali walikuwa pamoja kwenye bendi ya Yamoto Band.
Mbosso akiongea na Azam Tv amesema kwasasa hawako karibu kwasababu awali alikuwa anamsupport msanii huyo katika kazi zake ambazo amekuwa akizitoa lakini yeye alikuwa hasapotiwi.
"Baada ya kumsupport Aslay kwa muda mrefu watu wakawa wananaimbia mbona wewe unam-support halafu yeye haku-support? umem-follow mwenzako ameku-unfollow. Jifunze kubalance shobo, nikasema kumbe na mimi naonekana namshobokea ngoja na mimi nim-unfollow. Kwa hiyo sasa hivi kila mtu hana urafiki na mwenzake,” alisema Mbosso.