Misingi mitano (5) ya kuifanya ili uweze kuwa mbunifu

Ili uweze kuwa mbunifu unahitaji kufahamu mambo ya msingi ambayo ni vyema ukayabeba na kuayatendea kazi kila wakati, kwani neno ubunifu si kugundua kitu kipya pekee , bali ubunifu ni kitendo cha kuweza kuongezea thamani pia kitu au jambo la zamani.

Ifuatayo ndiyo misingi ya kuwa mbunifu:

1. Kufanya kitu ambacho unakipenda.
Kufanya kitu ambacho unakipenda kutoka nafsini mwako ni siraha tosha dhidi ya kufikia mafanikio  makubwa. Watu wengi wamekuwa katika hali ambayo haivutii machoni pa watu wengine au machoni pao  binafsi, hii ni kutokana na kufanya vitu ambavyo hawavipendi.

Ila ukweli ni huu ya kwamba ukifanya kitu ambacho unakipenda kitakupa hamasa za kutosha kila wakati na hatimaye kuwa mbunifu zaidi. Na endapo utafanya kitu pasipo kukipenda uwezekano wa kutenda jambo hilo kwa asilimia mia ni mdogo sana, hivyo kama unataka kuwa mbunifu hakikisha unafanya kazi kwa kuipenda.

2. Kufanya kitu kwa muda muafaka.
Kufanya kitu kwa muda muafaka ndiyo nguzo pekee ya kuwa mbunifu. Ubunifu ni lazima uweze kuwa sawa na maisha halisi ambayo watu wanaishi, kwa kuangalia nini wanahitaji nini zaidi. Kwa mfano kuna usemi unasema ya ugunduzi wa kitu kipya unafanya kitu kingine kife. Kwa mfano mtu aliyegundua matumizi ya laptop aliangalia changamoto zilizopo katika matumizi ya desktop. Na kufanya hivyo mgunduzi huyo alitambua watu wanahitaji nini na kwa wakati gani.

3. Fanya kitu mara kwa mara.
Ubunifu ni kufanya kitu kilele kwa njia tofauti, katika kila nyanja yeyote ile tunahitaji kuwa na ubunifu, na ubunifu wa jambo fulani husaidia kuongeza thamani ya kitu fulani. Hivyo ili kuwa mbunifu zaidi kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha unakuwa unalitenda jambo hilo mara kwa mara na kwa njia tofauti, na kufanya hivyo kutakusaidia wewe kuwa mbunifu.

4. Usiache kujifunza.
Kujifunza hakuna mipaka, hiyo ndiyo kauli inayotakiwa kudumu kila siku katika fikra zako. Nasema hivyo kwa sababu watu wengi tumekuwa wavivu sana wa kujifunza vitu vipya. Wengi wetu tunadhani kufanikwa katika maisha huenda ikawa labda ni miujiza.

Lakini ukweli haupo hivyo hata chembe, kwa kila sekta amnbayo ungependa kuwa mbunifu zaidi hakikisha unatumia muda mwingi kuweza kujifunza zaidi kuhusu eneo hilo. Huwezi ukasema unataka kufanikiwa na hili hali hutaki kuwa bora katika eneo hilo, kufanya hivyo itakuwa ni sawa na bure.

Lakini kabla sijatia nukta siku ya leo naomba nikole wino kwa kusema ‘ubunifu ndiyo roho ya mafaniko kwa kila sekta’’.

Mpaka kufika hapo afisa mipango sina ziada tukutane tena siku nyingine.

Ndimi: Benson Chonya