Umoja wa Mataifa chini ya uongozi wa Antonia Guterres hauungi mkono upande wowote kunako mzozo unaoendelea nchini Venezuela.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa Umoja huo hautounga mkono upande wowote ule katika mzozo unaoendelea nchini Venezuela kwa ajili ya kuwa mpatanishi.
Uamuzi huo ni kwa ajili ya kupatia ufumbuzi kunako mgogoro uliotokea nchini humo baada ya Juan Guaido kujitangaza kuwa rais wa mpito wa Venezuela.
Umoja wa Mataifa utashirikiana na wadua tofauti kutafuta suluhu katika mzozo huo.
Maandamano ya Janauri 23 ya upinzani na wanaomuunga mkono rais Nicolas Maduro yamepelekea sura mpya katika ukanda mzima Amerika Kusini.
Juan Guaido, kiongozi wa bunge la Venezuela alijitangaza kuwa rais wa mpito nchini humo katika mkutano wa upinzani.
Juan Guaido alitambuliwa kama rais wa Venezuela na Marekani, Australia, Canada, Colombia, Argentina, Costa Rica, Guatemala na bunge la Umoja wa Ulaya.
Kwa upande mwingine, Uturuki, Urusi, Cuba, China na Bolivia zinamuunga mkono rais Nicolas Maduro.
Marekani amesema kuwa itaidhibu serikali ya Maduro kwa kumkabidhi Juan Guaido milki za kampuni ya mafuta ya PDVSA.