.

2/14/2019

Mzee Akilimali afunguka kuhusu mchezo wa Simba SC na Yanga SC


Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga SC, Mzee Ibrahim Akilimali amefunguka kuwa anaamini wapinzani wao Simba SC watashinda kwenye mchezo wao utakaochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Simba na Yanga watachuana ikiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali wa Ligi Kuu Bara kumalizika bila ya kufungana.

“Sioni dalili za kuweza kupata matokeo kwenye mchezo huo, sioni kabisa nakwambia kwa sababu Simba wanapendwa na TFF ndiyo wanawabeba''. amesema Mzee Akilimali.

Mzee Akilimali ameongeza kuwa Simba wao wana kila kitu na timu yao ya Yanga inajiendesha kwa michango hadi kocha anatoa pesa yake mfukoni kuwalipa wachezaji, anaona wazi watafunga watakavyo.