Ndege mbili za kijeshi za India zaangushwa na Pakistan


Jeshi la anga la Pakistan limeziangusha ndege mbili za kijeshi za India baada ya kuvuka mpaka kati ya nchi hizo mbili hasimu zenye silaha za kinyuklia katika eneo linalogombaniwa la Kashmir leo, na kumkamata rubani mmoja wa India.

Hatua hiyo inayoongeza wasi wasi inakuja masaa kadhaa baada ya Pakistan kusema makombora yaliyofyatuliwa na vikosi vya India kutoka upande wa Kashimir unaodhibitiwa na India na kuwauwa raia sita na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Hata hivyo Msemaji wa jeshi la anga la India Anupam Banerjee mjini New Delhi amesema hana taarifa kuhusu taarifa hiyo ya Pakistan. Hapo awali afisa mwandamizi wa polisi wa India Munir Ahmed Khan alisema ndege ya jeshi la anga la India imeanguka katika sehemu inayodhibitiwa na India katika eneo la Kashmir na kwamba haikufahamika mara moja iwapo kuna watu waliofariki.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia