Ni vema kila mkoa kuwe na ofisi ya Mwanasheria Mkuu - Waziri Mkuu


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha inakuwa na ofisi zake katika  kila mkoa nchini.

"Kwa kuwa sasa mna muundo mpya na majukumu yenu yameongezeka yakiwamo ya uratibu na utoaji wa ushauri wa kisheria, itakuwa vema kuwa na ofisi kila mkoa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta au kuomba ushauri wa jambo la kisheria," Waziri Majaliwa alitoa wito huo juzi alipotembelea banda la ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika maonyesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika  viwanja vya  Mwalimu Nyerere 'Square' Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu alisema anaamini baada ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuundwa upya inakuwa na nafasi nzuri ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa tija.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items