Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa katika uongozi wake hajawahi kuingilia utendaji wa Bunge.
Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya Sheria ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC).
"Mimi nimejitahidi sana katika uongozi wangu kutokuingilia muhimili wowote, sijaingilia bunge hata wakizungumza kule wanakutukana sanasana unazima Tv , sijaingilia mahakama, ndio uhuru huo"
Aliendelea kwa kusema kuwa, 'Nitumie fursa hii kuwasihi wananchi kushirikiana na mahakama na vyombo vingine vya sheria, kusoma sheria japo kidogo na kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi,'.
