.

2/14/2019

Picha: Wananchi Simiyu wapiga kura ya siri kubaini wauaji


Wakazi wa Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega mkoani wamepiga kura ya Siri kuwabaini watuhumiwa  wa matukio ya mauji ya watoto mkoani humo.

Hivi karibuni watoto watatu wameuawa na sehemu zao za siri kunyofolewa mkoani Simiyu, kando ya Ziwa Victoria nchini,matukio yote ya Simiyu yametokea katika kata ya Lamadi wilaya ya Busega.