Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amefunga maadhimisho ya wiki ya Sheria ambapo amezungumzia mambo mbalimbali.
Maadhimisho ya wiki ya Sheria ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC).
"Kwa ndugu zangu wapelelezi, kapelelezeni haraka, mtu ameshikwa ameiba na kidhibiti anacho labda hata amefungiwa nacho shingoni, bado unataka ukapeleleze tu, unataka ukapeleleza alivyoiba alikuwa ameinama au amesimama," ameeleza.
Amesema matatizo ya ucheleweshaji kesi, ushahidi na kutotolewa kwa nakala ya hukumu kunapelekea wananchi kujichukulia Sheria mkononi.
"Ameshikwa na meno ya tembo upelelezi bado unaendelea, ameshikwa na madawa ya kulevya bado unaendelea, badala ya kumpeleka nayo na kumaliza haraka wanasema lazima tumpeleke kwa Mkemia Mkuu yanavyozidi kukaa huko wanasema ni majivu sio madawa ya kulevya," amesema.
Aliendelea kwa kusema kuwa, 'Makosa ya kukosa kuwajibika, kutokuwa waadilifu na kutotoa haki ni changamoto ambazo zimeendelea kuripotiwa kuwahusu watoaji haki katika Mahakama zetu, sisi sote kwa pamoja tutimize wajibu wetu katika kutoa haki,'.
