Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwaua Majambazi watatu waliokuwa na silaha ya moto ambayo bado haijafahamika ni silaha ya aina gani maeneo ya nyakabungo kata ya Isamilo, Wilaya ya Nyamagan, Mkoani humo
Tukio hilo limetokea Usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8 mara baada ya Askari Polisi kupokea taarifa toka kwa raia wema kwamba katika maeneo yao kunasikika milio ya risasi na kuvunjwa kwa Maduka.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Advera Bulimba amesema kuwa baada ya kupokea taarifa hizo Askari waliokuwa doria walifuatilia na kufanikiwa kufika eneo la tukio haraka.
Majambazi hao yalipohisi uwepo wa askari Polisi walianza kujihami kwa kuwarushia risasi hivyo askari wakaanza kujibu mashambulio hayo na kufanikiwa kuwauwa majambazi watatu.
Kutokana na taarifa kwa wananchi inasadikika majambazi walikuwa sita.
Majambazi hao hawakufanikiwa kuiba mali yoyote na hakuna madhara yoyote kwa wananchi.
Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hospital ya mkoa Sekou toure kwa uchunguzi na utambuzi na pindi uchunguzi ukikamilika itakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...........USISAHAU KUSUBSCRIBE............
