Msanii wa Bongo Fleva Young Killer amefunguka katika idadi ya nyimbo zake nyingi ni upi ambao akipata fursa anaweza kumsikilizisha Rais Magufuli.
Akizungumza kwenye kipindi cha The Bar Tender cha Wasafi TV amesema kuwa wimbo wake wa Dear Gambe ungemfaa zaidi Rais Magufuli kutokana na ujumbe wake.
"Wimbo ambao angeusikia akafurahi na akapenda, kwanza kabisa Dear Gambe kwa sababu ni wimbo ambao inpiration song ya watu wengi na unaweza ukaendelea kuishi milele kutokana na vitu ambavyo tumevizungumzia kule," amesema Young Killer.
Ameendelea kwa kusema, 'Watu wengi wanakunywa pombe na wataendelea kunywa pombe, so naamini Dear Gambe utaweza kumfaa kwa sababu kuna watu wanakunywa pombe na wanajutia,'.
