Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali ya mkoa huo imetenga eneo la hekari 15 kwaajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo utakaosimamiwa na TFF.
RC Gambo ameeleza hayo leo Jijini Arusha upofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho hilo.
"Serikali ya Mkoa wa Arusha Tumetenga hekari 15 kwaajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo na TFF ndio watakaousimamia bila kupata usumbufu," amesema RC Gambo.
Kwa upande wake aliyekuwa Rais wa TFF, Leodger Tenga amempongeza RC Gambo kwa hatua hiyo alichukua.
"Mheshimwa Gambo umeutendea haki mpira. Hilo wazo la kujenga uwanja ni wazo zuri sana. Nawaomba wakuu wa mikoa wengine waige wazo hilo la kujenga uwanja- Rais wa heshima wa TFF," amesema.
