Serikali kuwachukulia hatua wasambazaji wa taarifa za kichochezi mitandaoni


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametoa wito kwa wananchi kutojihusisha matukio ya watoto kuuwawa Njombe na matukio ya itikadi za kisiasa, imani za kidini au shughuli za kibiashara.

Akiwasilisha bungeni leo Jijini Dodoma taarifa ya Serikali kuhusu mauaji hayo, Lugola amesema Serikali imeshachukua hatua mbalimbali katika kutatua na kuzuia matukio hayo sanjari na kutoa maelekezo ya hatua za kupambana na uhalifu huo ikiwemo kuwatia mbaroni watuhumiwa.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali itachukua hatua kwa wale watakaojihusisha na vitendo vya usambazaji wa taarifa za kichochezi mitandaoni hivyo amewaasa Watanzania kuacha kusambaza taarifa za uzushi mitandaoni  kwa nia yoyote ile kwani ni takwa la Sheria ya Mtandao.

Hivi karibuni yamajitokeza matukio ya utekaji na mauaji ya watoto wadogo Mkoani Njombe, jambo ambalo limezua taharuki mkoani humo na nchini kote kwa ujumla.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items