Serikali yaongeza muda wa kuhakiki korosho za wakulima


Serikali imeongeza muda wa mwisho wa kufanya uhakiki wa korosho za wakulima hadi Februari 15 mwaka huu, kisha wataanza kulipwa stahiki zao.

Awali Rais Magufuli alikuwa ameagiza uhakiki na malipo viwe zimekamilika kabla ya Januari 31, lakini maelfu ya tani za korosho bado hazijahakikiwa.

Hadi kufikia January 30, 2019 Serikali imenunua jumla ya tani 214,269.684 za korosho ghafi zenye thamani ya Sh. 707,089,957,200.00 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji.

Juzi Bungeni Naibu Waziri wa kilimo, Omar Mgumba alisema jumla ya wakulima 390,466 wamekwisha lipwa  hadi kufikia January 30 mwaka huu, huku Vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa.