Taasisi za mwagiwa sifa kuunga mkono juhudi za Mahakama


Na.Timothy Itembe Mara.

Mahakama ya Wilaya Tarime mkoani Mara imemwagia sifa Taasisi mbalimbali ikiwemo maendeleo ya Jamii katika kuhakikisha mashauri ya Watoto yanasikilizwa na kumalizika kwa wakati kwa kuandaa taarifa muhimu zinazo hitajika kwa watoto wanaokuwa wamekinzana na sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo na Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime Rorya, Veronika Mugendi wakati akitoa hotuba mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Charles Kabeho wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambapo kiwilaya yamefanyika katika Viwanja vya mahakama hiyo.

Mugendi alisema kuwa maafisa ustawi wa jamii wamekuwa msaada mkubwa sana katika mahakama kuhakikisha mashauri ya Watoto (katika mahakama za watoto Juvanile Court) yanasikilizwa na kumalizika kwa wakati kwa kuandaa taarifa muhimu zinazohitajika kwa watoto wanaokuwa wamekinzana na sheria.

"Maafisa usitawi wa jamii pamoja na Asasi za kiraia zimekuwa zikitoa mchango mkubwa kama mdau wetu katika maswala mazima ya usimamiaji wa haki za Binadamu,asasi hizi nyingi zimejikita katika kupinga mambo mbalimbali yaliyokinyume na sheria ambayo jamii zetu zimekuwa zikiyakumbatia na kuyaendekeza kama vile maswla ya ukatili wa kijinsia,mila potofu za ukeketaji kwa watoto wa kike"alisema Mugendi.

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Tarime na Rorya, Kilulu Kulimba alisema kwa nyakati tofauti kuwa katika  gereza lake ipo haja serikali kuandaa na kujenga Gerza la Watoto kwasbabu gereza lake linapokea  watoto chini ya miaka 18 wanaokamatwa na kushitakiwa huku wakifikishwa katika Gereza hilo kuhifadhiwa na kutunzwa kwaajili ya kufikishwa mahakamani kusikiliza kesi zao.

Naye mkuu wa wilaya mpya wa Tarime,Charles Kabeho alisema kuwa mahakama inayohaki ya kutenda haki8 kwa kila mteja wao bila kubagua watu kwa jinsi zao ama umasikini walionao kwa hali hiyo watende kazi kwa weredi huku wakimwoogopa Mwenyezi Mungu pamoja na sheria za nchi zilizopo.









wa tutumia rasilimali zilizopo hususani Watu ambao ndio wadau wa mahakama katika kuwatenda haki huku jamii hiyo ikielimishwa kuhusu sheria kwa lengo la kupunguza msongamano mahakamani.