Watu 29 wakamatwa kwa mauaji ya watoto Njombe


Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa tamko la serikali bungeni kuhusu mauaji ya
watoto yanayoendelea mkoani Njombe.

Akizungumza leo Bungeni amesema kuwa hadi sasa watu 29 wanashikiliwa na jeshi hilo na tayari
timu ya wapelelezi imetumwa mkoani humo. 

"Hadi sasa hatua zilizochukuliwa na serikali, zimefanikisha kukamatwa kwa watu 29 kwa ajili ya
uchunguzi na mahojiano," amesema.

Ameendelea kwa kusema tayarii serikali imetuma timu ya wataalamu wa upelelezi kuvisaidia vyombo vya dola mkoani humo kuchunguza  matukio hayo kwa kutumia falsafa ya ulinzi shirikishi.

Kauli hiyo inakuwa zoikiwa ni siku kadhaa baada ya Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 kupatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.