Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa soko la kuangalia vyombo vya habari kutoka nje.
Rais Magufuli amesema kuwa watu waangalie lakini vyombo vya nchini vitoe muelekeo wa maisha ya Watanzania Milioni 55.
"Tanzania haiwezi kuwa ni soko la kuangalia vyombo vya habari kutoka nje, watu waangalie nje lakini vyombo vyetu viwe direction ya maisha ya Watanzania Milioni 55, vyombo vya nje kamwe haviwezi kuongelea positive maendeleo ya nchi yenu leo wataandika wamekufa wangapi," amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipotembelea Kituo cha Channel 10 ambapo ameahidi kukabidhi Mil 100 ifikapo kesho kwa ajili ya ununuzi wa vifaa.
