Watumishi 24,000 wahitajika mahakama za Tanzania


Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema kuwa ili Mahakama zote nchini ziweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi wanahitaji watumishi zaidi ya 24,000.

Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya Sheria ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC).

"Kutokana na shughuli za mahakama kusambaa kila kona nchini, mahitaji halisi ya watumishi ni makubwa mno, utafiti unaonesha kwamba ili mahakama zote nchini zifanye kazi kwa ufanisi kwa upande wa rasilimali watu watumishi 24 elfu 643 wanahitajika," amesema Prof.Ibrahim.

Katika hautua nyingine amesema Mahakama ya Tanzania imemuomba Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kuweka Sheria zote kwenye mtandao ambapo ameeleza jinsi Mahakama ilivyojipanga kutoa huduma kuendana na mabadiliko ya Teknolojia.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items