Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekiri kuwa baadhi ya mapadri
wakatoliki waliwadhulumu kingono watawa wa kanisa hilo mbali na hata kumbaka mmoja na kumweka kama mtumwa wa ngono.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Kanisa katoliki katika jimbo la Texas nchini Marekani
limewabainisha mapadre mia mbili na themanini wanaotuhumiwa kuwadhulumu kingono watoto.
Utakumbuka August mwaka jana Papa Francis alisema kuwa yupo upande walioathirika zaidi ya 300 waliofanyiwa ukatili wa kingono na baadhi ya makaasisi wa kanisa hilo katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.
