Waziri Kangi Lugola ayatilia shaka maelezo ya dereva wa Lissu

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amekuwa na mashaka na maelezo aliyoyatoa dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Ndugu Adam Bakari, kuhusu tukio kushambuliwa kwa risasi Mbunge huyo jijini Dodoma mnamo Septemba 7, 2017.

Kangi ameeleza kuwa  wanamtaka dereva wa Mbunge huyo awaeleze kwa nini alipoona wanafuatwa na magari mengine nyuma akiwa pamoja na mbunge huyo hakuchukua uamuzi wa kwenda kituo cha polisi kilichopo jirani ya nyumba aliyokuwa akiishi Lissu.

Kauli hiyo ameitoa, Kangi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Arusha ambapo amesema maelezo ya dereva huyo yanatia shaka.

"Kwa hali ya kawaida ni jambo la kushangaza risasi zote hizo wanasema 38, hata moja haikumpata dereva huyu,” amesema Lugola.

Kuhusu eneo hilo kuondolewa kamera za CCTV, Lugola amesema nyumba za Serikali jijini Dodoma hazina kamera hizo na huo ni upotoshwaji mkubwa ambao unalenga kuwadanganya wananchi na kuwataka waichukie serikali yao.

Lugola aliongeza kuwa "Ni vyema ni kwaambia Watanzania kuwa Mh. Tundu Lissu ni muongo kweli kweli, mimi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi nataka kuwaambia uongo wa Tundu Lissu.