DC Katambi na Mbunge Mavunde watatua kero za Maji na Umeme


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh Patrobas Katambi akiambatana na Mbunge Wa Jimbo La Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo wamefanya mkutano mkubwa wa wananchi katika kata ya Mbabala kusikiliza kero na kutatua changamoto za kero za Maji na Nishati ambazo zimekuwa zikiwabili wananchi wa eneo hilo.

Wakitoa maoni yao kwa niaba ya wananchi wengine Bi Sophia Machaka  na Bw Pancras Mpanda wamewaomba viongozi hao kusaidia usambazaji wa Maji katika eneo lote na kusaidia kuunganisha  umeme katika Zahanati na nyumba ya Daktari,lakini pia wananchi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kuwapelekea nguzo 19 za umeme kwenye kisima cha Maji zenye thamani ya Tsh 15,000,000 na kukifanya kisima hicho kutumia mfumo wa umeme.


Akijibu kero hizo Mh Mavunde amewaahidi wananchi hao kupeleka nguzo za umeme kesho siku ya Jumamosi na ifikapo wiki ijayo umeme utawaka katika zahanati na kuwajulisha kuwa watachimba visima viwili vya maji  katika kata hiyo mara baada ya kazi ya survey kukamilika.

Aidha Mkuu wa Wilaya Mh Katambi amewataka wananchi hao kulinda miundombinu yote ya maji na kutoa tahadhari kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika wanaharibu miundombinu hiyo na kukwamisha upatikanaji wa huduma,pia amemuagiza Mhandisi wa Maji wa Jiji Eng. Kirita kuhakikisha wanakamilisha kazi ya ujenzi wa vituo vya maji na usambazaji wake kwa wakati.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items