Zaidi ya wanakijiji 130 wauawa nchini Mali


Zaidi ya watu 130 wameuawa na watu wenye silaha kwenye kijiji katikati mwa nchi ya Mali na washambuliaji waliokuwa wamevalia mavazi ya kijadi ya uwindaji.

Watu wenye silaha walikizunguka kijiji hicho majira ya alfajiri kabla ya kuwashambulia watu katika makazi yao katika eneo la Ogossagou mjini Mopti.

Washambuliaji walikua wakiwalenga jamii ya Fulani ambao wanashutumiwa kuwa na uhusiano na wanamgambo.

Shambulio hilo lilijitokeza wakati mabalozi wa Umoja wa Mataifa walipokua nchini Mali kujadili ongezeko la machafuko nchini humo.

Ujumbe kutoka baraza la usalama la umoja wa mataifa ulikutana na Waziri mkuu Soumeylou Boubeye Maiga kuzungumza kuhusu ongezeko la vitisho kutoka kwa wapiganaji wa jihadi katikati mwa Mali, Wanakijiji walishambuliwa kwa ''risasi na mapanga'', shirika la habari la Ufaransa, AFP limeeleza, Mashuhuda pia wameiambia AFP kuwa karibu kila nyumba ya kijiji hicho zilichomwa moto.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items