Hali ni ya wasiwasi mkubwa kati ya Israel na Ukanda wa Gaza


Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mashariki ya Kati Nickolay Mladenov amelaani shambulizi la roketi liliwajeruhi watu saba katikati mwa Israel akisema halikubaliki, na amearifu kuwa Umoja wa Mataifa ulikuwa ukishirikiana na Misri katika juhudi za kujaribu kutuliza uhasama.

Hata hivyo amekiri kuwa hali bado ni ya wasiwasi. Jeshi la Israel limesema linasitisha shughuli zote za kilimo karibu na mpaka wa Ukanda wa Gaza na kuwataka raia wote wa nchi hiyo kuheshimu maagizo yake kwa muda usiojulikana.

Roketi la masafa marefu lililofyatuliwa kutoka Ukanda wa Gaza limeiharibu nyumba katika mji wa katikati mwa Israel usiku wa kuamkia leo, na kujeruhi watu saba, na tukio hilo limemlazimisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kufupisha ziara yake mjini Washington. Israel inalituhumu kundi la Hamas kufanya shambulio hilo, lakini afisa wa kundi hilo amezikanusha shutuma hizo katika mahojiano na shirika la habari la AFP.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items