Wauguzi Muhimbili watakiwa kufuata sheria


Wauguzi na wakunga Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa mbalimbali wanaotibiwa katika hospitali hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Muuguzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC), Gustav Moyo kwenye kongamano la siku moja linalofanyika katika Hospitali ya Muhimbili.

“Wauguzi na wakunga mnapaswa kuzingatia upendo na huruma kwa wagonjwa, ndugu na jamaa wa wagonjwa. Jambo muhimu mnatakiwa kuboresha mawasiliano na kuzingatia maandili na kuwaona ndugu wa wagonjwa ni  wadau,” amesema Moyo.

Pia aliwataka wauguzi na wakunga kutowatelekeza wagonjwa wakati wanapohitaji huduma kwa kuwa kumtelekeza mgonjwa ni kosa kwa mujibu wa sheria na hivyo amewataka kuzingatia sheria na kanuni za kazi ili kuboresha huduma mahali pa kazi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items