Polisi wa Comoro wafyatua gesi ya kutoa mchozi kuwatawanya wapinzani


Polisi katika visiwa vya Comoro wametumia gesi ya kutoa machozi kuwalitawanya kundi la wafuasi wa upinzani, wakati matokeo ya uchaguzi mkuu wa jana Jumapili yakitarajiwa kutangazwa. Rais wa sasa Azali Assoumani anapigiwa upatu kuibuka mshindi.

Watu wawili, mwandamanaji na askari kanzu wakati kundi la watu takriban 100 lilipoanza kuelekea katika viwanja vya uhuru katika mji mkuu, Moroni, wakidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na mizengwe.

Kundi kuu la upinzani limesema hitilafu katika uchaguzi wa jana ambazo ziliripotiwa na tume ya uchaguzi, zinaweza kuchukuliwa kama mapinduzi, na kuwataka wananchi kusimama kidete kupinga hali hiyo.

Afisa mmoja wa tume ya uchaguzi aliliambia shirika la habari la AFP hapo jana, kwamba vituo kadhaa vilihujumiwa wakati zoezi l kupiga kura likiendelea.

Vile vile mashahidi walizungumzia masanduku yaliyojaa karatasi za kura yaliyogunduliwa katika kisiwa cha Anjouan ambacho ni ngome ya upinzani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items