Hili lazima niliseme, jambo linanikera - Katibu Mkuu CCM


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amefichua namna tamaa ya madaraka kwa baadhi ya wahadhiri inavyoibua vita kubwa nyakati za kusaka viongozi na wakuu wa idara kwenye vyuo vikuu nchini.

Amesema kwenye michakato hiyo huibuka vikundi vya watu ambao hupanga safu kama chama cha siasa bila kuzingatia sifa uadilifu na ueledi wa kitaaluma. Dk.Bashiru ameyasema hayo jijini Dodoma wakati alipokuwa akiagwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Nchini (ASA).

“Hili lazima niliseme, jambo linalonikera kwenye taasisi za elimu ya juu ni kwa baadhi ya wahadhiri kuwa na tamaa ya madaraka pindi panapokuwepo mchakato wa kuwatafuta viongozi wa chuo au wakuu wa idara”amesema Dk.Bashiru.

Dk.Bashiru amesema kuwa alipokuwa UDSM michakato miwili ilifutwa kwa kuwa ilikuwa kichefuchefu. Amesema kuwa michakato ya aina hiyo ni lazima izingatie uwezo na uadilifu kitaaluma kwani viongozi wanaosimamia sekta ya elimu lazima wawe wenye sifa zenye ubora.