Umekuwa ukihangaika sana na kupambana vilivyo katika kutaka kuhakikisha kuwa unafanikiwa na unakuwa mwenye maisha bora au mafanikio ambayo unayataka, lakini pamoja na juhudi nyingi ambazo umekuwa ukiweka bado umekuwa ukijikuta hausongi mbele hata kidogo. Jambo hili laweza kusababishwa na vitu vingi sana lakini hapa nataka kukueleza kwa ufupi sana jambo moja tu ambalo linakufanya usisonge mbele, ambalo ni mipaka unayojiwekea katika akili yako na maisha kwa ujumla.
Binadamu kwa kawaida amekuwa ni mtu mwenye kujiwekea mipaka mingi sana katika akili yake, si semi kuwa ni vibaya kuweka mipaka katika akili yako lakini inategemeana na ni aina gani ya mipaka ambayo unajiwekea katika maisha yako. Kumbuka huwezi kufanikiwa kama mipaka unayojiwekea ni yenye kujaa wasiwasi, hofu na visingizio.
Yaani akili yako hapa unakuwa umeiwekea mipaka kuwa inakuwa inafanya kazi kwa baadhi ya mambo na baadhi ya mambo inalala. Mipaka yaweza kuwa pia ni ile hali ambayo ukitaka kufanya kitu linakuja wazo la achana na hilo jambo achana na hilo jambo, na unaachana nalo bila kujiuliza kwanini uachane nalo.
Mipaka mingine yaweza kuwa ni ile hali ya kuifanya akili yako kutokuona kuwezekana kwa jambo kwa kila kitu, yaani hapa wewe umejiwekea mipaka kwa kuitawaza akili yako na neno haiwezekani, ndio maana kila jambo ambalo unakuwa ukitaka kulifanya wewe unaona ni kama haliwezekani, hata kama linawezekana.
Sasa jambo hili ndilo limekuwa likikurudisha nyuma na kukufanya ubaki pale pale kwa kuwa akili yako imejaa neno haiwezekani haiwezekani na huu ni mpaka ambao umekuwa ukiwatesa watu wengi sana na kuwafanya waanze kuwaona baadhi ya watu kama wenye bahati, kubalikiwa, waajabu kuliko wao kumbe tatizo sio bahati au kubalikiwa tatizo ni mipaka wanayojiwekea wenyewe. Maana hao unaowaona ni kama wana bahati na wamebalikiwa hawajajiwekea mipaka ya haiwezekani bali wao huona fursa na wakaitumia fursa husika moja kwa moja huku wakiamini kuwa jambo fulani lawezekana hata kama litachukua muda au litawapitisha katika magumu gani kimaisha wao ambacho hutazama ni kutaka kuona kuwa wanachokitaka kimetimia.
Mpaka mwingine ni ile hali ya ngoja ngoja, yaani umeyajaza maisha yako na ngoja ngoja tena wakati mwingine umekuwa ukiendelea kuihararisha hiyo ngoja ngoja yako kwa methali na misemo kama vile, “polepole ndio mwendo”, “haraka haraka haina Baraka”, “mwenda pole hajikwai”, “subira yavuta heri” n.k. kwa kuwa umetawaliwa na ngoja ngoja nyingi hivyo umekuwa mzito wa kufanya maamuzi hata kwa jambo ambalo linatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka na hii imekupelekea sasa ushindwe kufanikiwa maana umekuwa na nyingi ngoja ngoja kuliko vitendo halisi. Sina maana kuwa ukurupuke sasa na uanaze kupalamia kila unachokiona hapana nachotaka hapa ni wewe kuifanya akili yako ichemke na iweze kufanya upembuzi yakinifu haraka haraka ndani ya muda mchache na uweze kuwa umepata majibu fasaha.
Mpaka wa mwisho ni kutokukubali mabadiliko, kuna watu huwa wanapenda kwenda kinyume na wakati au nyakati, yaani wao huwa wanataka kubaki pale pale hata kama kuna mabadiliko yalishatokea na mifumo ya vitu imebadilika lakini wao hutaka kubaki pale pale kwa misemo yao ya “old is Gold”. Sasa kuwa makini sana maana dunia inabadilika sana kila siku kama utabaki pale pale hii inaaama hautafanikiwa na kusonaga mbele.
Hiyo ni mipaka michache ambayo umekuwa ukiiweka katika akili yako na inakurudisha nyuma. Anza kuitoa sasa.

Tags:
makala