Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi amezuru Rwanda na leo ametembelea eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbari jijini Kigali.
Ziara hii imekuja, wiki mbili kuelekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kutokea kwa mauaji hayo mabaya yaliyotokea mwaka 1994 na kusababisha zaidi ya watu 800,000 kupoteza maisha. Hii ni ziara ya kwanza kwa rais Tshisekedi baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa DRC. Rwanda na DRC ni mataifa jirani ambayo yanashirikiana kibiashara lakini suala la usalama mipakani linasalia changamoto.
Kwa upande mwengine rais wa Rwanda Paul Kagame, ameishtumu Uganda kwa kuiwekea vikwazo vya kufanya biashara, suala ambalo amesema linakwenda kinyume na makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
