Wabunge 100 wa Ujerumani na wa Ufaransa wameanza kikao cha pamoja mjini Pairs hii leo. Spika wa Bunge la Shirikisho la Ujerumani Wolfgang Schäuble amewataka washiriki wa kikao hicho kufanya mjadala uliochangamka, hata ikiwa ni kuhusu masuala tete.
Mwenzake wa bunge la Ufaransa Richard Ferrand amesisitiza kuhusu hali ya mpya ya ushirikiano, ambao ameuita kuwa ni wa mfano kwa bara la Ulaya.
Schäuble na Ferrand wametia saini sheria ya kuanzisha kikao hicho kidogo cha pamoja cha wabunge wa nchi zao, ambacho kitakuwa kikifanyika angalau mara mbili kila mwaka.
Miji ya Berlin na Paris itakuwa ikibadilishana zamu kuvipokea vikao hivyo.
