Dayna Nyage awafunda wasanii wenzake


Msanii wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amewataka wasanii kujikubali waposhuka kimuziki kwani kuna kupanda na kushuka.

Muimbaji huyo amesema wasanii wawe na tabia ya kuwekeza kwenye maisha yao mengine, wawe na kiasi ambacho wanaweza kujiwekea, kwani wasanii wengi wanaokuwa na msongo wa mawazo kwa kuwa hawakuwa na mipango ya kujiwekea akiba.

"Unajua stress za wasanii zinatokana na kutetea jina lake au nafasi yake pale ambapo mambo yanapokuwa hayaendi yaani umeshuka kisanii halafu akatokea msanii akafanya vizuri kuliko wewe,’’ amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Siamini kama stress zinasababisha vifo hiyo ni hatua ambayo kila mtu ataipitia, Mungu ndiye anayejua, ila zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya, mbona kuna wasanii wanaopitia magumu sana na wamepitia stress nyingi na kubwa sana lakini muda wao haujafika na mpaka leo wapo na wanaendelea vizuri.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items