Jibu la Rais Magufuli baada ya kuombwa leo iwe siku ya mapumziko


Rais Magufuli amekutana na timu ya Taifa mara baada ya ushindi walioupata kwenye mechi iliyochezwa jana ya  kufuzu michuano ya Afcon kwa kuifunga timu ya Uganda mabao 3 bila.

Rais Magufuli katika hotuba yake leo alipowaita Taifa Stars na Mpiganaji, Hassan Mwakinyo Ikulu kwa ajili ya chakula cha pamoja amesema kuwa amepita kwenye mitandao ya kijamii ameona namna ambavyo Watanzania wamefurahia ushindi huo na kuomba leo kuwa siku ya mapumziko.

"Sikushangaa kuona wengine wamelewa ndio furaha na Watanzania wanapenda furaha,”amesema Rais Magufuli.

"Wengine walikuwa wanasema kwanini usitangaze kesho ikawa mapumziko, nikasema Watanzania na mapumziko jamani, ila sikushangaa ndiyo dhana ya kufurahi, ” aliongeza Rais Magufuli.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items