Mabadiliko ya Hali ya Hewa yawashtua Wakulima Kagera


Na. Clavery Christian, Bukoba

Wakulima Mkoani Kagera wametahadharishwa na kushauliwa kushirikiana na maafisa ugani ili kuweza ku baini mazao ambayo yanastahimili jua kutokana Na mabadiliko ya Hali ya hewa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Mkoani Kagera, Bw, Steven Malundo wakati akizungumza na Muungwana Blog ofisini kwake na kusema kuwa kwa msimu huu wa mvua zitakuwa za wastani kuliko vipindi vingine.

Malundo, ameongeza kuwa kwa upande wa Mkoa Kagera kuna baadhi ya maeneo yatapata upungufu wa mvua kama kibondo na maeneo mengine yatakuwa na mvua wastani na kuwataka wakulima katika maeneo yote ya Mkoa wa Kagera kulima mazao yanayostahimili jua kali kama vile viazi, Mihogo na Magimbi.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items